Akiba na Amana
Akiba ya Lazima
Pesa inayowekwa na mwanachama ili kumuwezesha kupata mkopo. Kila mwanachama atatakiwa kuweka Akiba kila mwezi kiasi kisichopungua shilingi 20,000/= au kiasi kingine kadiri itakavyoamuliwa na mkutano mkuu. Mwanachama anaweza kupunguza Akiba yake ikiwa hana mkopo wowote na kwa kufuata taratibu zilizowekwa na chama. Pia chama kinalipa riba juu ya Akiba alizoweka mwanachama kwa mwaka. Akiba ni lazima kwa mwanachama, kwa kila mwezi. Mwanachama akiacha uanachama atarudishiwa Akiba zake zote.
Akiba ya Hiyari
Akiba ya Elimu
Pesa inayowekwa na mwanachama kwa ajili ya kumsaidia kujiendeleza kielimu, yeye au mtegemezi wake. Chama hupokea na kutunza Akiba za wanachama kupitia makato kwenye mishahara au kuweka Benki kiasi chochote Zaidi ya makato anayokatwa katika mshahara wake. Pia chama kinalipa faida juu ya Akiba alizoweka mwanachama kwa mwaka. Mwanachama akiacha uanachama atarudishiwa Akiba yake yote.
Akiba ya Mtoto
Pesa inayowekwa na mwanachama kwa ajili ya maendeleo ya mtoto kwa miaka ya baadae. Pia chama kinalipa riba juu ya Akiba ya mtoto iliyowekwa chamani kwa mwaka. Mwanachama akiacha uanachama atarudishiwa Akiba yake yote
Amana
Ni kiasi chochote cha fedha anachoweka mwanachama muda wowote na
kutolewa au kupunguzwa muda wowote wa masaa ya kazi. Amana za
wanachama zitatunzwa au kuwekekwa sehemu ya usalama kama
ilivyoelekezwa na sheria, kanuni na sera inayohusika, na sehemu kubwa
zitawekwa benki.
Faida juu ya Amana zitalipwa kwa kiwango kilichoainishwa kwenye Sera
husika au kiwango kingine kitakachopitishwa na Mkutano Mkuu.