Bodi ya ELIMU SACCOS LTD inawakumbusha kuweka Akiba kila mwezi, kukopa na kufanya marejesho kwa maendeleo ya SACCOS yetu.

Matangazo yote na Matukio Mbalimbali

MIKOPO YA KARADHA

Tunapenda kuwataarifu wanachama wote kuwa huduma ya mikopo ya vifaa sasa inapatikana. Unaweza kupata mkopo wa vifaa mbalimbali kulingana na mahitaji yako. Vifaa vinavyo patikana ni pamoja na:-
vifaa vya umeme TV, FRIJI, MASHINE YA KUFULIA, AIR CONDITION (AC) NK
vifaa vya usafiri PIKIPIKI, BAJAJI, GARI
vifaa vya vyumbani FURNITURES NK
vifaa vya biashara na matumizi mengine.
Wanachama wote wanaotimiza vigezo wanakaribishwa kuwasilisha maombi yao.
kwamaelezo zaidi na utaratibu wa kupata mkopo, tafadhali wasiliana na ofisi ya mikopo.
KARIBU UCHANGAMKIE FURSA HII NA KUBORESHA MAISHA NA SHUGHULI ZAKO.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2026-05-26 13:01:43

🔥 MZIGO MPYA UMEWASILI! 🔥

Tunawaletea SESCOM Electric Pressure Cooker – jiko la kisasa linalorahisisha maisha yako jikoni! Inaokoa muda wa kupika
Inatumia umeme kidogo (energy saving)
Inapika vyakula mbalimbali: wali, maharage, nyama, supu ya kongoro
Rahisi kutumia na salama kwa familia
Ubora wa hali ya juu + Warranty ya miaka 2
💥 Bei nafuu kabisa – njoo ujipatie kabla hazijaisha!

👉 Tunakopesha kwa wanachama wetu
👉 Au ukija na mwanachama kama mdhamini unapata kwa mkopo pia

laki na hamsini 150,000 kwa cash
laki na stini 160,000 kwa mkopo.
wote mnakaribishwaaaaaaa

Imetolewa na: Mwenyekiti 2026-04-09 13:25:21

MABORESHO YA MASHARTI YA CHAMA MWAKA 2025

Kupata masharti ya chama toleo la mwaka 2025 Pakua hapa.
Toa maoni yako Hapa

Imetolewa na: Mwenyekiti 2024-10-25 15:09:09

MABORESHO YA SERA YA MIKOPO MWAKA 2025

Kupata sera ya mikopo iliyo huishwa mwaka 2025 Pakua hapa.
Toa maoni yako Hapa

Imetolewa na: Mwenyekiti 2024-10-25 14:57:10

Mafunzo ya Wanachama

Bodi ya ELIMU SACCOS LTD inawatangazia wanachama kuwa kutakuwa na mafunzo kwa wanachama wote tarehe 01/06/2024 kuanzia saa 2:30 asubuhi, katika ukumbi wa Bwalo la Umwema. Aidha Bodi inaomba upatapo taarifa hii umtaarifu na mwenzako karibuni sana.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2024-04-23 11:48:25

Mafunzo ya wawakilishi

Bodi ya Elimu SACCOS Inawatangazia wawakiishi wote wa vituo kuwa kutakuwa na mafunzo siku ya tarehe 10/02/2024 kuanzia saa 2 asubuhi katika ukumbi wa CWT Mkoa wa Morogoro. Unaombwa kuja na Majina na namba ya NIDA ya kila mwanachama katika kituo chako.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2024-02-03 09:12:17

Mkutano Mkuu

Mwenyekiti wa ELIMU SACCOS LTD anawatangazia wanachama wote kuwa, kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Wanachama wote utakaofanyika tarehe 18/11/2023 katika ukumbi wa Atubellah - Modeco kuanzia saa 02: 00 Asubuhi, tafadhali naomba wote tuhudhurie, karibuni sana.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2023-10-30 08:48:30

Uchaguzi wa Viongozi

Mwenyekiti wa Elimu SACCOS anawatangazia wanachama wote uwepo wa nafasi za kugombea uongozi wa chama kwa ngazi ya; Wajumbe wa Bodi, Kamati ya Usimamizi na Mwakilishi wa wanachama. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 04/10/2023 karibuni sana.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2023-09-26 05:46:55

SESCOM Pressure Cooker

ELIMU SACCOS Inawatakangazia wanachama wote huduma mpya ya mkopo wa Jiko la kisasa kutoka kampuni ya SESCOM linalotumia umeme kiduchu kupika vyakula vyote. Keshi ni Tsh 160,000/= na mkopo ni Tsh 180,000/=, Kwa maelezo zaidi karibuni ofisini kwetu.

Imetolewa na: Kamati ya Uwekezaji 2023-06-20 08:13:37

Marejesho ya Mkopo

ELIMU SACCOS LTD inawakumbusha Wanachama wote wenye Mikopo kufanya Marejesho ili kuepuka usumbufu kwao na kwa wadhamini wao. Aidha Wanachama wengi hawafanyi marejesho kwenye Mkopo wa Dharura na wengine hawaheshimu Starding Order zao.

Imetolewa na: Kamati ya Mikopo 2023-04-08 13:41:53

Uchaguzi wa Wawakilishi wa Vituo

Bodi ya Elimu SACCOS inapenda kuwatangazia wanachama wote wenye sifa za kungombea nafasi ya uwakilishi ngazi ya vituo kuchukua fomu na kuzirudisha kabla ya 20/04/2023. Fomu zinapatikana kwa wawakilishi wa sasa , Kwenye Mfumo na Ofisini, Karibuni.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2023-04-05 05:09:38

Nafasi ya Ajira

Bodi ya ELIMU SACCOS inawatangazia nafasi ya Ajira ya Mhasibu, kwa maelezo zaidi wasiliana na mwakilishi wa wanachama katika vituo vya kazi au tupigie kwa namba hizi: 0653492956 na 0684113743. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12/02/2023 saa kumi jioni.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2023-02-06 06:55:20

Riba juu ya Akiba

Mwenyekiti wa Elimu SACCOS anawatangazia wanachama wote kuwa Riba juu ya Akiba kwa mwaka 2021 imetoka. Hivyo tuwasiliane na Wawakilishi ili kujua kiasi ulichopata kulingana na Akiba uliyokuwanayo Desemba 31, 2021.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2023-02-01 08:24:04

Marejesho ya Mkopo

ELIMU SACCOS LTD inawakumbusha Wanachama wote wenye Mikopo kufanya Marejesho mapema ili kuepuka usumbufu kwao na kwa wadhamini wao. Aidha Wanachama wengi hawafanyi marejesho kwenye Mkopo wa Dharura na wengine hawaheshimu Starding Order zao.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2022-12-19 07:06:48

Pata Asali Mbichi

Ndugu Mtendeje Kingimali anapenda kuwatangazia wanachama wote wa Elimu SACCOS kuwa anauza Asali Mbichi . Lita moja Tshs 11,000/= na nusu lita Tshs 5,500/= naomba tumuunge mkono mwenzetu kwa mawasiliano zaidi piga namba 0754260808 Asante.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2022-11-19 16:11:09

Mkutano Mkuu wa 17

Wanachama wote mnakaribishwa kwenye Mkutano Mkuu wa 17 utakaofanyika tarehe 05-11-2022 katika ukumbi wa Bwalo la Umwema Morogoro kuanzia saa Mbili na nusu asubuhi. Pia mnakumbushwa kuzingatia muda. Asante

Imetolewa na: Mwenyekiti 2022-10-05 09:28:50

Uzinduzi wa Website

Mwenyekiti anawataarifu kuwa kwenye Mkutano mkuu wa tarehe 05/11/2022 tutakuwa na uzinduzi wa Website yetu ya chama utakaofanywa na mgeni rasimi, karibuni sana wanachama na wadau wote wa ELIMU SACCOS LTD.

Imetolewa na: Web admin 2022-10-05 08:30:42

Hisa kwa Wanachama

Wanachama wote mnakumbushwa kumalizia Hisa za Msingi kama tulivyokubaliana kwenye mkutano mkuu uliopita kuwa kila Mwanachama anatakiwa kumalizia Hisa za Msingi kabla ya tarehe 30/10/2022, Asanteni.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2022-10-04 14:45:05

Uwekezaji wa Uwakala

Ndugu mwanachama wa Elimu SACCOS unakumbushwa kutumia huduma yetu ya uwakala kwa kutoa,kuweka na kulipia Mikopo yetu ili kuleta tija kwa chama chetu.

Imetolewa na: Mwenyekiti 2022-09-20 10:20:45