Uanachama
Sifa za Uanachama
"Mtu yoyote anaweza kujiunga na chama endapo atakidhi mahitaji ya Fungamano la pamoja la uanachama na sharti awe na sifa zifuatazo;"
- Awe mwenye umri wa miaka isiyopungua 18.
- Awe Mwalimu wa Idara ya Elimu Sekondari, Msingi, Vyuo au mtumishi Kada ya Elimu katika Manispaa ya Morogoro.
- Awe mwenye tabia nzuri, mwaminifu na mwenye akili timamu
- Chama/Taasisi/Shirika lenye sifa za kujiunga na chama hiki kwa mujibu wa sheria ya vyama ya ushirika, Kanuni za vyama vya ushirika pamoja na masharti haya.
- Awe amelipa kiingilio, hisa za uanachama na kuweka akiba kwa kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa masharti haya na awe tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za chama.
- Awe anaelewa na kuwa tayari kutekeleza madhumuni ya chama kama yalivyoainishwa kwenye masharti haya na kufafanuliwa katika nyaraka mbalimbali.
- Awe tayari kufuata masharti ya chama, kanuni na sheria za vyama vya ushirika wakati wote.
- Asiwe mwanachama wa SACCOS nyingine.
- Asiwe na shughuli yeyote ile inayofanana na kuweka au kukopesha wanachama ili kuondoa mgongano wa masilahi.
Taratibu za kujiunga na chama
- Maombi ya uanachama yatafanywa kwa kujaza fomu ya uanachama kwa kupitishwa na Bodi na baadaye kuidhinishwa na mkutano mkuu wa chama.
- Fomu ya maombi itakuwa na maelezo ambayo yatatiwa saini na mwombaji na kuthibitisha kuwa amesoma masharti haya na anakubali kuyafuata.
Mwanachama atakapokubali kujiunga na Chama atapaswa:-
- Kulipa kiingilio kitakachokuwa kimepangwa na Mkutano Mkuu
- Kununua idadi ya hisa kumi na tano (15) zenye thamani yashilingi 20,000/= kwa kila hisa. Kwa kuanzia mwanachama anaanza kwa kununua hisa tatu (03) kwa mkupuo na hisa12 zilizobaki atapaswa kuzilipa katika kipindi cha miezi sita (06). Ukomo wa Hisa kwa mwanachama ni Hisa 400.
- Kuweka Akiba kila mwezi isiyopungua shilingi 20,000/= kwa ajili ya
maendeleo yake na pia anaweza kuitumia kama dhamana ya mkopo.
1. Mwanachama ambaye atashindwa kutimiza matakwa ya sharti dogo (1) (b) hapo juu hataruhusiwa kunufaika na haki za mwanachama katika chama.
2. Viwango vya kiingilio, hisa na akiba vinaweza kubadilishwa kwa maamuzi ya Mkutano Mkuu.
3. Mwanachama aliyekamilisha kulipia Hisa zote atapewa hati ya kumiliki Hisa.
-
Wajibu wa Mwanachama
- Kukamilisha kununua hisa na kuweka akiba kwa kuzingatia Masharti ya chama;
- Kufuata na kutekeleza Sheria ya Vyama vya Ushirika na Kanuni zake, Masharti ya chama, maamuzi ya Mkutano Mkuu na maelekezo mengine halali kwa mujibu wa Sheria za nchi;
- Kurejesha mkopo kwa wakati uliopangwa;
- Kutoa michango mbalimbali katika kuendeleza madhumuni ya chama kadri itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu;
- Kubeba dhamana endapo janga lolote litakipata chama;
- Kuwa mwaminifu na kuonesha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za chama;
- Kumdhamini mkopo mwanachama mwenzake isipokuwa kwamba mwanachama aliyedhamini hatakuwa na haki ya kudhaminiwa na mwanachama aliyemdhamini katika kipindi kile kile;
- Kulipa mkopo alioudhamini endapo mdhaminiwa/mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake; na
- Kuhudhuria semina na mafunzo yanayotolewa na Chama.
-
Haki za Mwanachama
- Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano yote inayohusika;
- Kushiriki katika kutoa uamuzi wa mambo mbalimbali katika Mikutano Mikuu;
- Kupiga kura chini ya misingi ya mtu mmoja kura moja bila kujali idadi ya Hisa anazomiliki;
- Kuchagua na/au kuchaguliwa katika Uongozi wa chama.
- Kuwa na haki sawa kuhusu mali ya Chama na kudhibiti ipasavyo matumizi yake;
- Kupatiwa huduma zozote zinazotolewa na chama ilimradi amekidhi masharti yanayoambatana na huduma hiyo;
- Kupatiwa taarifa mbalimbali za shughuli za chama, muhtasari wa mkutano na nyaraka nyingine za chama kwa ajili ya mapitio akiwa katika ofisi za chama;
- Kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na Kanuni zake pamoja na masharti haya;
- Kuteua Mrithi;
- Kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya Bodi ya Uongozi na Mkutano Mkuu;
- Kupokea gawio na faida nyingine kutoka katika shughuli za chama kwa kuzingatia masharti; na
- Kupewa kitabu cha akiba au kifaa kingine chenye makusudi hayo.